Zverev aondolewa michuano ya Mexican Open

Zverev aondolewa michuano ya Mexican Open

Mchezaji namba 3 kwa ubora katika mchezo wa tenisi duniani na bingwa wa Olympic, Alexander Zverev ameondolewa katika michuano ya Mexican Open.

Zverev ameondolewa katika michuano hiyo baada ya kuipigiza raketi yake na kuigonga kwenye miguu ya mwamuzi huku akitoa lugha chafu za matusi akimlaumu msimamizi huyo kwamba ameharibu mchezo.

Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Ujerumani amefukuzwa kwenye michuano hiyo ya wazi ya Mexico kwa kitendo cha kugonga kiti na miguu ya mwamuzi huyo akiwa anarudi kukaa kwenye kiti chake baada ya mchezo kumalizika.

Pia alipigiza raket yake mara tatu kwa nguvu na hasira katika miguu ya mwamuzi anayekaa juu katikati ya uwanja usawa wa wavu baada ya kufungwa seti mbili kwa alama 6 - 2, 4 - 6, na 10 - 6 dhidi ya Lloyd Glasspool.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags