Zuchu: Natamani kuzaa na Diamond ila hajatia ubani

Zuchu: Natamani kuzaa na Diamond ila hajatia ubani

Mwanamuziki wa #BongoFleva, Zuchu, aonesha hisia zake za dhati kwa kutamani kuzaa mtoto na #DiamondPlatnumz lakini akiwa ndani ya ndoa.

Zuchu ameyasema hayo kupitia Instastor yake akiwa ame-share picha na kuandika ujumbe wa kumsifia Diamond kuwa ni baba bora kwa watoto wake hali ambayo imemfanya na yeye atamani kuzaa na mwanamuziki huyo ila kwa sharti la kumuoa.

"Kukutazama ukiwa na watoto wako kunanifanya nitamani kuwa na mtoto na wewe, Ila ndo hivyo hujatia ubani sekhee," Ameandika.

Ikumbukwe kuwa Diamond kwa sasa ni baba wa watoto kadhaa ambapo amekua akionekana kuwaonesha upendo na kuwajali watoto wake jambo ambalo linamvutia Zuchu na kutamani kuanzisha familia na mwanamuziki huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags