Zuchu Kupanda Jukwaani Na Dogo Paten Leo

Zuchu Kupanda Jukwaani Na Dogo Paten Leo

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Zuchu ameweka wazi kuwa atapanda jukwaani na msnii wa singeli, Dogo Paten kwenye ‘Samia Serengeti Music Festival 2025’ inayotarajia kufanyika usiku wa leo Aprili 26,2025 katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es salaam.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Paten ameshare voice note aliyotumiwa na Zuchu ikimtaka ajiandae kwa ajili ya show hiyo huku msanii huyo akitoa shukrani kwa Zuchu kwa sapoti anayompatia.

“Asante Sana Dada Yangu Ila Ukweli Sina Chakusema Dada Yangu Kwa sapoti Kubwa Unayonionesha Pia Napenda Kushukuru Uongozi Mzima Wa Wa Wasafi Pia Mashabiki Zangu Badaye Inshaallh Tukutane Tanganyika Peckers Kawe,” amendika Dogo Paten

Aidha kupitia voice note hiyo Zuchu amesikika akisema “Paten Mdogo wangu leo kuna show ile ya Kawe pale muda wangu wa kupanda nikiwa namaliza session yangu nikiwa kwenye nyimbo yangu ya mwisho nakupandisha. Unatakiwa uzingatie mazingatio ya kuuwa kwenye hii show

Nataka ukipanda pale uuwee yaani tukitoka pale nataka habari iwe moja wewe na hii itakuwa ndio safari yako inaanza, sasa kaa na DJ wako sijui utafanya mazoezi vipi, fanya mazoezi vizuri tengeneza confidance yako muome Mwenyezimungu wako na kama hauna mavazi njoo nyumbani mapema nimeshamwambia mtu atakuletea nguo kila kitu utakikuta hapa,”amesema Zuchu

Hata hivyo aliongezea kwa kusema “Kwahiyo relax lakini nataka ukifika pale uuweee tukitoka pale iwe ndio safari yako yaani nyimbo imefanya vizuri lakini pia ukawaoneshe watu kwamba mimi nina uwezo sio kwamba nabebwa tuu. Sasa hii ndio safari yako inaanza ukiamua kucheza mwenyewe haya lakini leo mimi nakupandisha jitahidi sana urelax,”

Ikumbukwe wawili hao tayari wanakolabo ya pamoja iitwayo ‘Afande’ ambayo promo yake imekuwa ikifanya vizuri katika mitandao ya kijamii hasa TikTok.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags