Zuchu amwagia sifa Diamond, Amshukuru Chris Brown

Zuchu amwagia sifa Diamond, Amshukuru Chris Brown

Baada ya mwanamuziki wa Marekani Chris Brown ku-share video kupitia mtandao wake wa TikTok akicheza ngoma ya ‘Komasava’ ya Diamond, msanii Zuchu amemwagia sifa Simba kwa kuendelea kulipaisha taifa la Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zuchu ame-share video hiyo ya Brown ikiambatana na ujumbe wa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kuipeperusha bendere ya tasnia ya muziki wa Bongo.

“Hatuwezi kuigiza kusema kama hii sio jambo kubwa, kweli hili ni jambo kubwa sio tu kwa Diamond bali kwa taifa zima la Waswahili na Afrika kwa ujumla” ameandika Zuchu

Aidha aliendelea kwa kumsifia Diamond kwa kuipeperusha bendera ya tasnia na kulifanya Taifa kutembea kifua mbele huku akimshukuru Chris Brown kwa kuendelea kusapoti wasanii wa Afrika.

“Taifa letu na Afrika kwa ujumla siku zote itakuheshimu kwa kuwakilisha utamaduni wetu vizuri Mr Brown”
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags