Mwanamuziki anayetamba na albumu ya ‘Peace of Money’ Zuchu amemtolea povu kaka wa mwanamuziki Diamond, Ricardo Momo baada ya kufunguka kuhusiano na Zuchu kutamani kuolewa na Simba.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Zuchu ameweka wazi kuwa kwa upande wake sio lazima yeye kuolewa na Diamond na wala hajalazimisha uhusiano huo.
“Embu naomba nitoe tamko sina haja wala silazima mimi kuolewa na Nasibu ifike hatua mutafute vingine vya kuhoji, hana lazima hata ya kua na mimi sijawahi kumshikia bastola wala kumteka ana haki ya kwenda kokote anakoridhika. Maana naona mmeacha kazi mnafanya kazi mpya kudiscredit na kutafuta comments na likes barua yenu ya wazi.
“Kama rahisi sana kumng’ang’ania ambieni hao mnaotaka awe nae wakang’ang’anie tuone, kubwa sijaliona nazaliwa na mamaangu tayari maarufu hamuoni kumaliza redio wala ndugu zangu au watu wangu kuongelea jambo moja kuchaa basi fanyeni hivi,” amesema Zuchu
Mbali na hilo amewataka watu hao wanaoendelea kuzungumza kuhusiana na uhusiano wao wamshauri Simba aachane naye huku akitishia kumpeleka mtu mahakamani.
“Mshaurini aniache muone kama ntamfata na mabomu embu choreni mipaka sio kutwa kujifanya mnanimudu sasa nasubiri nione this time napeleka mbwa mahakamani kutwa ndoa ndoa, ndoa, hatuli vikashuka,” amemalizia Zuchu
Utakumbuka kuwa kupitia kipindi cha Mashamsham Momo alifunguka kuwa msanii huyo hatakiwa kulazimisha kuolewa na Diamond kwani huenda Mungu hajapanga wao kuwa pamoja.
Leave a Reply