Zuchu album ‘Cover’ iko tayari

Zuchu album ‘Cover’ iko tayari

Baada ya mwanamuziki Zuchu na mzalishaji wa muziki Trone kuthibitisha ujio wa albumu ya msanii huyo kuwa imekamilika kwa asilimia 100, sasa Zuchu ameweka wazi kuwa cover ya album hiyo iko tayari na huenda ikaachiwa muda wowote kuanzia sasa.

Ukiwa ni muendelezo wa Update ya albumu ya Zuchu kupitia instastory yake ameandika kuwa cover ya albumu hiyo imekamilika. “My Album Cover done”.

Mpaka kufikia sasa Zuchu ametoa taarifa ya ujio wa albumu lakini bado hajaweka wazi tarehe rasmi ya kuachiwa kwa albumu hiyo.

Endapo albumu hiyo itafanikiwa kuachiwa itakuwa ya kwanza kwa Zuchu. Mwaka 2020 mwanamuziki huyo alifanikiwa kutoa EP yenye nyimbo saba ambayo ndiyo iliyomleta mjini.

EP hiyo ya Zuchu iliyopewa jina la ‘I Am Zuchu’ ikiwa na nyimbo kama ‘Hakuna Kulala’, ‘Nisamehe’, ‘Wana’, ‘Ashua’, ‘Kwaru’, Raha’ na ‘Mauzauza aliyomshirikisha Mama yake Khadija Kopa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags