Zingatia haya kabla ya kujiajiri

Zingatia haya kabla ya kujiajiri

Mambo vipi kijana mwenzangu ! ni wasaa mwingine tena tunakutana katika kujadili mambo mbalimbali yanayohusu  kazi, ujuzi na maarifa.

Leo ndani ya magazine ya Mwnanachi scoop nimekuandalia mambo ya kuzingatia kabla ya kujiajiri mwenyewe binafsi.

Ungana nami kwenye makala haya ili uweze kupata elimu zaidi juu ya masuala ya kujiari kwani itakusaidia pia katika kufanya maamuzi kwenye karia yako.

Kujiajiri mwenyewe jambo jema sana kutokana na tayari utakua unafanya kazi zako vile unavyotaka na unavyopenda mweneyewe katika muda ambao wewe unaona ni mwafaka kwako bila kushurutishwa.

Hata hivyo unapaswa kufahamu mambo muhimu ya kufanya kuzingatia kabla hujaamua kuingia katika uwanja huo wa ajira binafsi twende sawa hapa.

Jambo la kwanza kabisa na lamuhimu unapaswa kuzingatia suala zima la Nidhamu.

Suala la nidhamu pamoja na bidii‚Ä®Vinahitajika kwa kiasi kikubwa sana kwani hakutakua na  boss wa kukusimamia na kukupangia majukumu yako.

 Hivyo basi  wewe mwenyewe ndio kila kitu unatakiwa ujitume na umalize kwa wakati unaotakiwa na katika kiwango bora kukidhi mahitaji ya wateja.


Jambo la pili ni suala zima la Mtaji  kwani ndiyo kitu muhimu  sana maana huwezi kuanza biashara yoyote au mradi bila mtaji, cha muhimu ni kuanza mradi wako kutokana na fedha ulizo nazo, au kama ni mkopo tafuta mahali wanopotoa mikopo yenye marejesho nafuu itakusaidia pia wakati wa kurejesha kulingana na biashara utakayoanzisha.


Suala la mauzo ni jambo lakuzingatia pia kwani   Mkakati wa mauzo uko hivi ili  wateja waweze kununua huduma au bidhaa zako lazima uwe na utaalam wa kutangaza bidhaa zako na kutafuta masoko.

Hivyo ni lazima ujifunze mbinu mbalimbali na kujielimisha jinsi ya kujitangaza bidhaa zako  na ujipange jinsi utakavyo ongeza mauzo kila siku katika shughuli zako.

Lamuhimu na lakuzingatia kwenye maisha ya karia yako kijana mwenzangu tambua kwamba kama umeajiriwa usiache kazi kabla hujajipanga au kupata sehemu nyingine.


Ikiwa umeajiriwa na unataka uache kazi ufanye shughuli zako binafsi, usiache kazi kwa kukurupuka, anza mradi wako huku bado uko kazini jipe muda wa kujipanga na kuangalia, mradi wako unavyoenda ukiona imeshasimama na inaenda vizuri hapo unaweza acha kazi, unendelee na shughuli zako binafsi.

Kubwa zaidi unapaswa kutambua kuwa Ajira binafsi ni nzuri ukiwa nayo ila inachangamoto zake pia hivyo suala la uvumilivu linahitajika kwa kiasi kikubwa sana.

Ushauri wa bure pia  anza mradi wako kutokana na ujuzi na mtaji ulionao, pia unahitaji kujituma, kuweka nidhamu katika kazi kujitoa na kuwasikiliza wateja wako nini wanapenda na nini hawataki kutoka kwako ukizngatia hayo  utafanikiwa mtu wangu wa nguvu.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post