Zijue mascara na namna ya kuipaka

Zijue mascara na namna ya kuipaka

Unapochagua mascara kuna mambo muhimu ya kuzingatia kulingana na lengo lako unalotaka kutimiza. Unatakiwa kujua unataka kope zionekane ndefu(lengthening), zionekane zimejaa/nene (thickening), zisishikane na je ukinawa na maji mascara itoke au laa (water proof).

 Wengi tunanunua tu mascara kwa wamachinga nk bila kujua itafanya nini ilimradi ukipaka kope zinaonekana.

 Ya Kurefusha kope, hii kibrashi chake kina vinyweleo vingi ili ifikishe mascara vizuri kwenye kope hasa katika ncha za kope. Urefu wa kope hutengenezwa na namna mascara inavyofika vizuri kwenye ncha (tips) za kope. Unapopaka mascara katika kope hakikisha ncha za kope umezifikia vizuri. Unaweza usibandike kope za bandia lakini mascara ikakubeba ukaonekana na kope ndefu.

 Ya kujaza kope, hii huwa na kibrashi ambacho ni rahisi kufikisha mascara katika shina la kope zako kuzipa ujazo. Na pia unaweza kuzifanya zijae kwa kuziviringisha katika brashi yako. Hakikisha imeandikwa volume/ thickener: mara nyingi zimetengenezwa na nta flani na kemikali aina ya silicone ambavyo hufanya kope kuwa zimejaa.

Mascara zisizojirundika na kunatisha kope, hii huwekwa viungo vya silk na glyserini, pia kibrashi chake huwa kirefu na vinyweleo virefu ili mascara ikolee kwa kulingana katika kope.

Waterproof Mascara, hizi huwekwa viungo maalumu vinavyoweza kukinga unyevunyevu usiathiri kipodozi chako. Kwa hiyo mascara hii haivurugiki kirahisi ukipaka. Lakini saa nyingine viungo vyake huwa vina ukali hivyo ni vyema ukapaka kope zako vaseline kabla ya kupaka ili kope zisikatike.

 Pamoja na yote hayo, angalia bajeti yako iko vipi ili kujipatia unachoweza kumudu na ambacho kinatimiza lengo. Inasemekana saa zingine sio kemikali tu za kwenye mascara bali pia aina ya kipakio chake huweza kuleta matokeo mazuri.

Unaona tofauti ya kope kulingana na brashi zilivyo? Brashi huja za namna tofauti kama hivi wingi wa vinyweleo vya brashi na urefu huamua urahisi katika upakaji wake, mfano ili uweze kupaka vizuri kwenye ncha za kope unahitaji brashi ndefu yenye vinyweleo vingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags