Zijue faida 14 za kufanya tendo la ndoa

Zijue faida 14 za kufanya tendo la ndoa

Mark Lewis

Tendo la ndoa ni hali ya kukutana kimwili kati ya mwanaume na mwanamke. Tendo la ndoa ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba watu wengi wanapenda kuwa na mwenza ambaye wanaridhishana katika tendo la ndoa. Jarida lako pendwa la Mwananchi Scoop linakuletea nakala kuhusu faida za tendo la ndoa.

  1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo:

Wanawake ambao hufika kilele  angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi.

  1. Huongeza ukakamavu wa mifupa:

 Wanawake waliokoma kupata hedhi ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya  oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis.

  1. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume:

Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.

  1. Hupunguza maumivu:

 Kufikia kilele (orgasm) wakati wa kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi.

  1. Hupunguza msongo wa mawazo:

Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam ambayo hufanya mwili kupumzika na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. 

  1. Huongeza kinga ya mwili: 

Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.

  1. Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini:

Ikiwa litafanyika baina ya wapendanao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana huongeza kujiamini.

  1. Kudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida:

Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao hawafanyi kabisa.

  1. Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini:

Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.

  1. Kuongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga.

Hivi husaidia kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke na hivyo kumwepusha na  maambukizi katika njia cha mkojo maarufu kama UTI. 

  1. Inaboresha uzazi

Kufanya tendo la ndoa kunaboresha uzazi, tafiti  zinaonyesha kuwa wingi wa tendo la ndoa, huchochea ongezeko la ubora wa manii.  Kwa hivyo, muda mrefu bila kufanya tendo la ndoa husababisha ubora wa shahawa kuzorota.

  1. Huongeza muda wa kuishi

Sio tu kwamba tendo la ndoa la mara kwa mara hufurahisha, inakusaidia kuishi kwa muda mrefu. Tafiti zinaonesha kuwa watu ambao walifanya tendo la ndoa angalau mara tatu kwa wiki, walipata hadi 50% nafasi ndogo ya kufa kutokana na ugonjwa wowote.

  1. Boresha hali yako ya mwili

 Dakika 30 za kufanya tendo la ndoa kuchoma hadi kalori 213 kwa wanawake na 276 kwa wanaume. Pia staili tofauti zinazotumika wakati wa kujamiiana husaidia kutanuka na kulegea kwa misuli.

  1. Husaidia kulala vizuri

Tendo la ndoa husaidia kulala vizuri kwa sababu inaweza kutufanya tujisikie uchovu zaidi baada ya kujamiiana, na pia huchochea uzalishaji wa melatonin. Kazi za neurochemical hii inayojulikana zaidi ni kwamba inachangia kushawishi usingizi mzito. 

HATARI ZA KIFO CHA GHAFLA WAKATI WA TENDO LA NDOA.

Hata hivyo wale wanaofanya tendo la ndoa wanaweza kuwa katika hatari ya kupata kifo cha ghafla, au wote wanaweza kupata maambukizi au kuugua wakati wa tendo hilo. wataalamu wa masuala ya tiba wameelezea mambo yanayoweza kusababisha mtu kufa wakati wa tendo hilo, iwe kwa wanawake au wanaume.

Yafuatayo ni mambo matatu yanayoweza kusababisha mtu kufa wakati wa kujamiiana.

  1. Matumizi mabaya ya dawa:

Wanaume mara nyingi hutumia dawa za kitamaduni au miti shamba ili kuwasaidia kuwa thabiti wakati wa tendo hilo.

  1. Maradhi ya moyo:

Matatizo ya kiafya sio jambo linalopaswa kupuuzwa inapokuja katika suala la kushiriki mapenzi

Mtu mwenye historia ya ugonjwa wa moyo anaweza kufa wakati wa tendo hilo kwasababu moyo wake utafanya kazi ngumu kuliko wakati wa kawaida

  1. Matumizi ya kupindukia ya dawa za kuongeza nguvu za kiume

Dawa ya Viagra imekuwa ikiuzwa katika maduka mbali mbali ya dawa duniani, kwa lengo la kuwasaidia wanaume hususani wenye magonjwa yaliyoathiri nguvu zao za kiume kuweza kurejesha uwezo huo.Kulingana na wataalamu dawa hii inapaswa kutolewa na Daktari kwa vipimo vinavyohitajika kulingana na tatizo lenyewe la kiafya.

Hatahivyo kutokana na upatikanaji kwa njia rahisi wa dawa hizi, baadhi ya vijana na wanaume wamekuwa wakizinunua kiholela kwenye maduka ya dawa na kuzitumia ili kuwaridhisha wapenzi wao. Kulingana na wataalam matumizi yasiofaa ya dawa hizi yanaweza kusababisha matatizo ya moyo na hivyo kuweza kuchochea kutokea kwa kifo wakati wa tendo hilo.

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags