Zijue chaguzi za serikali za wanafunzi vyuoni

Zijue chaguzi za serikali za wanafunzi vyuoni

Na Michael Anderson

Niccolò Machiavelli , katika kitabu chake maarufu ‘The Prince’, aliandika kama kiongozi hawezi kuogopwa na kupendwa kwa wakati mmoja, ni afadhali aogopwe kuliko kupendwa.

Uongozi ni mamlaka au karama ya kuwaonesha watu njia kwa vitendo. Kipimo cha uongozi ni jinsi gani anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.

Kiongozi bora hana muda wa kulalamika bali anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi au watu walio chini yake vile vile kiongozi wa kweli akiongea, watu husikiliza.

Kwa upande wa vyuo kuna Serikali za wanafunzi ambazo ni sehemu ya kujifunza na kuandaa viongozi vijana wa Taifa hili, uchaguzi ndiyo njia pekee ya wazi na haki inayowapa viongozi wa chuoni mamlaka kwa mchakato huo.

Leo tutaangazia namna mchakato unavyofanyika vyuoni katika kupata viongozi bora.

SIFA ZA KIONGOZI ANAYETAKIWA KUWAONGOZA WASOMI CHUONI
i. Awe na ufahamu wa tasisi husika
Kiongozi ni lazima awe na ufahamu mkubwa juu ya taasisi anayoiongoza, malengo yake, mazingira na matatizo yake mfano chuo husika
ii. Awe mwaminifu.
Kila taasisi huwa na lengo la kufikia shabaha fulani. Ni wajibu wa kiongozi kuwaongoza wanataasisi ili wafikie malengo yao. Kwa hiyo kiongozi ni lazima aweze kubuni mikakati na mbinu zitakazoiwezesha taasisi anayoongoza kufikia malengo yake.

iii. Awe na maadili mema.
Kiongozi ni lazima akubalike katika jamii na taasisi anayoiongoza. Ili akubalike hana budi kuzingatia maadili ya msingi ya jamii na taasisi yake. Mtu muongo, mlevi, mvivu, asiye mwaminifu n.k. hawezi kuwa kiongozi mzuri.
iv. Mcha Mungu.
v. Awe anakubalika na wanafunzi wenzake.
vi. Awe anaongoza watu katika misingi bora ya uongozi bila kujali jinsia, rangi, dini wala kabila. Awathamini watu wa makundi yote chuoni walemavu na wasio walemavu
vii. Awe anakubali kushauriwa ua kupokea ushauri kutoka kwa wengine mfano office za dean of students (walezi)
viii. Awe na uwezo wa kujifunza kutoka kwa watu wengine waliofanikiwa, awe na mawazo ya mbele ya kuona tatizo na kuonesha baadhi ya njia za kulitatua, pamoja na kuona fursa kwa ajili ya wanafunzi wenzake kwanza (first priority).

MCHAKATO WA KUWAPATA VIONGOZI VYUONI
Mchakato ni kama ilivyo kwenye katiba zinazowaongoza ni mchakato unaozingatia kanuni, sheria na taratibu chuoni, muundo wa uongozi upo kama ilivyo Serikali Kuu, Bunge, au Mahakama kwa baadhi ya vyuo mchakato huanzia bungeni, kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.

Tume kuruhusu uchukuaji wa forms lakini pia votting inafanyika screening na baada ya hapo majina kupelikwa Utawala Mkuu wa Chuo na kurudishwa kwa ajili ya kampeni kwa waliopita ambao huwa ni team mbili zilizofanya vizuri katika screening za utawala mkuu wa chuo.
Baada ya kampeni tume itaendesha mchakato wa kupiga kura kwa wanafunzi wote wanaotambulika chuoni na kisha tume ya uchaguzi ndiyo wenye mamlaka ya kutangaza washindi hadharani kwa wale waliopigiwa kura nyingi.

CHANGAMOTO ZA CHAGUZI ZA VYUO
Rushwa
Hii ni changamoto kubwa sana katika chaguzi na hata rushwa ya ngono inahusishwa kwa baadhi ya vyuo ili kupata viongozi , lakini rushwa kubwa ipo katika mchakato hususani tume za uchaguzi vyuoni ni sehemu kubwa ya rushwa na kupelekea kufutwa kwa chaguzi.

Haki kukosekana
Watu kupokea rushwa husababisha haki kukosekana mfano tume ya uchaguzi ikipokea rushwa watamtangaza mtu aliyetoa rushwa na siyo aliyeshinda kwa kura nyingi.

Udanganyifu wa taarifa
Hii hutokea sana katika mchakato, kimsingi katiba za serikali za wanafunzi vyuoni huelekeza uhalali wa kuwa viongozi mfano kuwa mbunge lazima uwe na GPA isiyopungua 3.5 kwa baadhi ya vyuo lakini wajanja hawakosekani kwa kudanganya taarifa ili kupata kile wanachokihitaji

NOTE: ewe kiongozi wa serikali ya wanafunzi chuoni amini kwamba cheo ni dhamana kwa maana hiyo unashikilia mamlaka unayopewa kwa muda na kuyaachia pale muda unapokuwa umekwisha, upo katika mfumo wa kiuendeshaji wa kupokezana vijiti vya nafasi za uongozi.
Usitumie cheo chako chuoni kuwa sehemu ya kuishi maisha bora na kusahau dhima kubwa iliyokupeleka chuoni mwishowe KUFELI MASOMO YAKO.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags