Ziiki yakanusha tuhuma za Diamond

Ziiki yakanusha tuhuma za Diamond

Kampuni ya Usambazaji Muziki ya Ziiki Media imetoa maelezo na kukanusha malalamiko ya mwanamuziki Naseeb Abdul Diamondplatnumz yaliyodai kuwa kampuni hiyo imewazuia kuachia leo wimbo wa mwanamuziki Lavalava uitwao 'Kibango'.

Kupitia taarifa hiyo iliyotolewa na Ziiki imeeleza kuwa taarifa ya kuachiwa kwa wimbo huo wameipokea tofauti na walivyokubaliana ambapo kimkataba msanii anatakiwa kuwasilisha wimbo walau wiki tatu kabla ya kutoa au kukiwa na sababu zilizo nje ya iwezo wake wanaweza kumpa walau siku saba ili wimbo uweze kutoka.

Hivyo basi Ziiki wanaeleza kuwa wimbo huo unaolalamikiwa wa Kibango uliwasilishwa siku ya tarehe 16.4.2024 na kutaka utolewe siku ya tarehe 19.4.2024 ambapo kwa hali ya kawaida iko nje na utaratibu uliokuwa umepangwa.

Pia wameeleza kila mara wamekuwa wakiwaelewesha wasanii wengi hasa kutoka Tanzania juu ya utoaji kazi kwenye Digital Platforms zote. Hivyo basi wamekanusha taarifa za kuzuia wimbo huo kama ilivyoelezwa na msanii huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags