Zari huenda akafunguliwa kesi ya unyanyasaji

Zari huenda akafunguliwa kesi ya unyanyasaji

Afisa mkuu wa polisi Uganda, Jackson Mucunguzi, ameweka wazi kuwa Shakib Lutaaya anaweza kumfungulia kesi ya unyanyasaji wa kisaikolojia mke wake Zarinah Hassan ‘Zari’.

Kupitia ukurasa wa X (zamani twitter) wa Mucunguzi amefichua kuwa endapo Shakib atapata ujasiri na nguvu anaweza kufungua kesi ya unyanyasaji wa kiuchumi na kisaikolojia.



“Ikiwa kaka yangu Shakib kama mtu mzima atajikusanya ujasiri na kujua haki zake, kesi ya ukatili wa kiuchumi na kisaikolojia wa nyumbani inaweza kusajiliwa katika Idara ya Ulinzi wa Watoto na Familia, na kusikilizwa kwa mafanikio katika mfumo wa haki wa Uganda” ameandika Jackson Mucunguzi

Hii inakuja baada ya Zari kushare video kupitia mitandao ya kijamii akitoa maneno ya udhalilishaji kwa Shakib. Utakumbuka kuwa ugomvi wa wawili hao unakuja baada ya Zari kumkaribisha Diamond nyumbani kwake Afrika Kusini kwa ajili ya kusheherekea siku ya kuzaliwa ya binti yao Tiffah.

Hata hivyo sio mara ya kwanza kwa wawili hao kutengana mwanzoni mwa mwaka 2024 wanandoa hao waliripotiwa kutengana huku kila mmoja akimu-unfollw mwenzake kupitia kurasa zao za Instagram na Shakib kurudi kwao Uganda, lakini wiki chache baadae walirudiana tena.

Zari na Shakib walifunga ndoa Oktoba 3, mwaka jana nchini South Africa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags