Zanzibar kuadhimisha miaka 59 ya mapinduzi yaliyouondoa utawala wa Sultani

Zanzibar kuadhimisha miaka 59 ya mapinduzi yaliyouondoa utawala wa Sultani

Hakika Visiwa vya bahari ya Hindi vya Zanzibar leo vinaadhimisha miaka 59 ya mapinduzi yaliyofanyika Januari 12 mwaka 1964 kwa kuuangusha utawala wa sultani kiasi mwezi mmoja tangu visiwa hivyo vilipojipatia uhuru kutoka kwa Uingereza.

Mwaka huu hakutakuwa na sherehe rasmi kuadhimisha siku hiyo na badala yake fedha zilizotengwa kwa ajili ya hafla ya taifa zitatumika kufadhili miradi ya maendeleo.

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu viongozi wa Zanzibar wamekuwa wakifungua miradi kadhaa ya kijamii ikiwemo shule, hospitalini na masoko kuelekea kilele cha siku ya mapinduzi.

Mapinduzi ya mwaka 1964 yaliongozwa na vuguvugu la chama cha Afro-Shirazi kilichokuwa kinaupinga utawala wa sultani Jamshid na serikali iliyoundwa na vyama vya ZNP na ZPPP.

Hata hivyo Miezi mitatu baada ya mapinduzi hayo, visiwa vya Zanzibar viliungana na iliyokuwa dola ya Tanganyika kuunda taifa jipya la Tanzania.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags