Zamu ya Burna Boy kupewa heshima Marekani

Zamu ya Burna Boy kupewa heshima Marekani

Mji wa Boston, Massachusetts nchini Marekani umetangaza Machi 2, kuwa ni siku ya Mkali wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria Burna Boy, itayoitwa ‘Burnaboy Day’ kama heshima kwa mwanamuziki huyo.

Barua ya kutangazwa kuwa siku hiyo imetolewa na kusainiwa na Ruthzee Louijeune, ambaye ni diwani wa jiji hilo.



Barua hiyo imeeleza kuwa wanampa Burna Boy heshima hiyo kutokana na kuurudisha muziki na sauti ya Kiafrika katika mstari, kupinga dhana potofu kuhusu wasanii wa Kiafrika na kuutangaza muziki wa Afrobeat ulimwenguni kote, hata hivyo, Burna alisifiwa kufungua milango kwa wasanii wenzake wa Kiafrika wanaotamani kufanikiwa.

Aidha imeonekana kuwa kufuatiwa na show pamoja na kazi zake Burna amekuwa na sauti ya kutetea haki za watu waliotengwa, kuburudisha, kuelimisha na kuhamasisha.

Maendeleo haya yanakuja siku chache baada ya Burna Boy kuujaza Uwanja wa Scotiabank uliyoko Toronto katika show yake ya hivi karibuni.

Hii siyo mara ya kwanza wa wasanii wa Nigeria kupewa heshima nchini Marekani ikumbukwe Meya wa Atlanta mwaka 2023, alitangaza Novemba 18 iwe siku ya mwanamuziki Davido ‘Davido Day’ kama heshima kwa msanii huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags