Zamaradi: kushindwa kwa wasanii wetu ni furaha

Zamaradi: kushindwa kwa wasanii wetu ni furaha

Kutokana na baadhi ya mashabiki kutoka nchini #Nigeria kuumizwa na kitendo cha mastaa wao kutopokea tuzo yoyote ya #Grammy, mtangazaji Zamaradi Mketema ameyatoa ya moyoni huku akiwataka wananchi wa Tanzania kuiga uzalendo wa watu wa #Nigeria.

#Zamaradi kupitia Instastory yake ame-share ujumbe mzito uliokuwa ukieleza

“Msanii wa #Nigeria akikosa tuzo ama hata kushindwa kwenye shindano lolote unayaona kabisa maumivu ya Wanaigeria, wananchi wao huumia kutoka moyoni, Njoo huku kwetu sasa msanii akikosa Tuzo ama shindano lolote ndio unapoishuhudia wazi kabisa furaha ya Watanzania.

Kiufupi kushindwa, kwa wasanii wetu ni furaha na vigelegele kwetu huku vicheko na maneno ya dhihaka yakisindikiza kushindwa kwao hivi somo la Uzalendo limekuwa gumu kiasi hiki #Tanzania? Wenzetu wamewezaje na sisi tulirogwa na nani?”


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post