Zaidi ya wanawake 60 watumiwa kondomu zilizotumika kwenye bahasha

Zaidi ya wanawake 60 watumiwa kondomu zilizotumika kwenye bahasha

Polisi kutoka nchini Australia wanachunguza kisa kimoja baada ya wanawake wasiopungua 65 kupokea kondomu zilizotumika kwenye bahasha.

Barua hizo, ambazo pia zilikuwa na jumbe zilizoandikwa kwa mkono, zilitumwa kwa anwani za kusini-mashariki na mashariki mwa Melbourne.

Wanawake wote wanaaminika walisoma shule ya kibinafsi ya wasichana ya Chuo cha Kilbreda mnamo mwaka 1999. Huku Polisi wakiamini kuwa waathiriwa ni sehemu ya shambulio lililolengwa.

Kwa mujibu wa gazeti la Herald Sun la Melbourne liliripoti kwamba wanawake hao wanashuku kuwa anwani zao zilipatikana kutoka kwa kitabu cha mwaka cha shule.

Aidha uchunguzi unaendelea na polisi wamemtaka yeyote mwenye taarifa kujitokeza. Wanatarajiwa kutoa Taarifa zaidi kuhusu kesi hiyo baadaye Jumatano.

Ikumbukwe tu Chuo cha Kilbreda, shule ya wasichana ya Kikatoliki inayojitegemea, ilianzishwa na Brigidine Sisters mnamo 1904 na ina wanafunzi wapatao 900 waliosajiliwa


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post