Yemi awasihi mabinti kuolewa na watu sahihi

Yemi awasihi mabinti kuolewa na watu sahihi

Mwanamuziki kutoka nchini #Nigeria #YemiAlade amewashauri wanawake wasio na waume kuhakikisha wanafunga ndoa na wenzi sahihi na kuachana na mashinikizo kutoka kwa familia au marafiki. 

#Yemi ameyasema hayo katika mahojiano yake na #CoolFM kwa kueleza kuwa hata yeye kwa sasa familia yake inampa shinikizo la kuolewe lakini inamuwia vigumu kupinga kwa sababu anaambiwa na watu anao waheshimu, hivyo basi anaamini ikiwa wana muamini basi watamvumilia ili aweze kupata mtu sahihi.

Licha ya hayo amedai kuwa sasa ni mwisho wa mwaka na watu wengi wanaolewa hivyo basi anawasihi mabinti wasifanye maamuzi mabaya ya kuolewa na wenzi wasio sahihi.

.

.

#mwananchiscoop

#burudikanasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags