Yajue matumizi ya Simu kitaaluma

Yajue matumizi ya Simu kitaaluma

Makala hii ilianza wiki iliyopita na leo tunaendelea nayo kipande kilichobakia hivyo msomaji wetu endelea kuwa nasi.

Basi Sikatai kwamba simu ya mkononi ni kwa ajili ya matumizi binafsi ya mtu.

Na kila mtu ana utashi wa kujiwekea mipaka ya watu wa kuwasiliana nao.

Lakini iwapo umeweka namba yako ya simu kwenye CV yako na kuisambaza hapo hakuna tena faragha, yaani privacy na unapaswa kila simu inayoingia uipokee kwa hekima na busara kwa kuanza kujitambulisha ili kuepuka kupoteza muda kuulizwa maswali lukuki yasiyo na tija.

Kumbuka huyu anayekupigia simu siyo kwamba anakupia simu wewe peke yako. Unaweza kukuta ana lundo la CV za watu wengi na ana muda mfupi wa kuwapigia na kuwaalika kwenye usaili.

Wenzetu wanasema first impression is last impression. Kwamba muonekano wa kwanza ndiyo tabia yako halisi.  Hayo marekebisho utakayoyafanya baadaye ukishajua unaongea na nani ni kujifaragua tu lakini tabia yako halisi hujitokeza awali unapokutana na mtu usiyefahamiana naye.

Binafsi ninapokutana na watu wenye tabia ya namna hii ya kupokea simu kizembe huwa najitambulisha na kuwasema na kisha kuwajulisha kwamba hawafai hata kuitwa kwenye usaili.

 Kama mtu hataki mawasiliano na watu asiyowafahamu na anatafuta kazi basi awe na simu mbili. Moja iwe ni ya faragha zake na hiyo nyingine iwe ni ya kutafutia kazi ili akipigiwa anaipokea kwa nidhamu.

Upokeaji wa simu kinidhamu ni ile tabia ya kujitambulisha mara tu baada ya kupokea simu ili kumfanya mpigaji ajue anaongea na nani.

Kwa mfano simu inaita na kupokea kwa kusema....

'Hallo Shaban anaongea... '

Au kwa kiingereza.

'Hallo, this is Shaban...'

Kwa kusema hivyo tu umemrahisishia mpigaji kuwa na uhakika kwamba amempigia mtu sahihi

Naomba niulize hususan kwa wanawake, Hivi ukitaja Jina lako kwenye simu unapungukiwa na nini? 

Kwa sababu hata baadhi hivi vikampuni vidogo ukipiga simu mapokezi unaweza kumsikia binti anapokea simu na kutaja jina la kampuni kisha basi na ukimuuliza jina lake yeye anataja jina la kampuni na kuuliza labda unataka kuongea na nani.

Mpaka unajiuliza hata kama hawakusoma hivi hawaangalii senema za wenzetu au hata tamthilia waone wenzetu wanavyo behave huko maofisini.

Na tabia hii ya mabinti wa hivi vikampuni vidogo kuwa na that kind of attitude zinakosesha kampuni fursa za biashara bila waajiri wao kujua na hivyo kampuni kukosa mapato.

Nazungumzia vikampuni vidogo kwa sababu hakuna kampuni kubwa inayoweza kuvumilia ujinga huo. 

Katika moja ya kampuni niliyowahi kufanya wakati fulani kuna kampuni iliajiriwa kwa ajili ya kufanya test call yaani simu ya majaribio ili kupima viwango vya upokeaji wa simu kitaaluma yaani Professionalism.

Na kila simu ilikuwa inarekodiwa na baada ya kumaliza mazungumzo na mteja aliyepiga kufanya test call walikuwa wanatuma alama ulizo score na sauti yako. Ili Kama Ulikuwa rude inakula kwako.

Ninavyofahamu mimi ni kwamba mtu wa mapokezi anapotaja jina lake kwenye simu mpigaji anahisi ukaribu na kujenga imani kubwa na kampuni husika hususan kwenye customer service.

Sasa uje hatua nyingine labda baada ya binti kupokea simu na kujitambulisha na kumweleza kuhusu nafasi ya kazi.  Jaribu kumwambia ajieleze kwa kifupi hapo hapo kwenye simu kuhusu historia yake fupi kitaaluma kwa kiingereza.

Utashangazwa na namna atakavyojieleza na hata kwa kiswahili utasikia vitu vya ajabu sana. Tena unaweza kukuta unaongea na graduate aliyemaliza Chuo hivi Karibuni.

Hawa ndiyo vijana wetu na wasomi wetu wa leo. Hawajui hata kujieleza kitaaluma kwa kifupi tu.

Wenzetu waliotutangulia kwenye teknoloji wanajua kujiongeza. Wao wanatengeneza sentence chache zinazowatambulisha kitaaluma na kuzikariri ili hata akiamshwa usingizini anajua aseme nini kuhusu yeye. 

Wenzetu wanajua kujiandaa na wako exposed na ulimwengu unaowazunguka kuhakikisha kila fursa inayowajia wanaitendea haki.

Hii inawahusu pia wafanyabiashara wadogo hususan hawa wa mitandaoni....

Naamini kuna jambo mmejifunza.

 


Comments 3


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Shaban Kaluse

A Sales and Marketing in the hospitality Industry and also a freelance journalist, writing about love and relationships and educative articles which aims for youths, every Tuesday on Mwananchi Scoop.


Latest Post