Yajue matumizi mbadala ya camera ya simu yako

Yajue Matumizi Mbadala Ya Camera Ya Simu Yako

Niaje mdau wa Mwanachi scoop!! Leo ndani ya smartphone bhana nakuletea Matumizi sahihi ya camera  zetu mbali na kupiga picha, wengi tumezoea camera  kuitumia kwa kupiga picha lakini ukweli wa mambo ni huu hapa nakupa leo uufanyie kazi.

Kuna matumizi mengi sana ya Camera ya simu janja zetu ukiachana nayale tuliyoyazoea ya kupiga picha tu, unaweza kuitumia kwa matumizi mengine kabisa yakarahisisha maisha yako twende sawa.

Scan nyaraka

Hii unaweza kabisa camera ya simu janja yako pia inaweza ikawa ina scan nyaraka tofauti tofauti, unaweza jiuliza kivipi hili? Usihofu fuatilia maelezo.

Pata picha unakuwa na scanner ambayo ipo mfukoni kwako unaweza uka scan vitu kama vile mikataba, risiti au kitu chochote kilichopo katika karatasi na unataka ukifanye kiwe kidigitali.

Baada ya hapo unaweza ukaamua kuvituma vitu hivyo katika barua au unaweza ukavihifadhi katika mfumo wa PDF au JPG.

Unataka kuscan vitu sasa? Kwa ios shusha(download) Evernote

Kwa Android shusha Google Drive ndani yake kuna kipengele cha ku’scan’

  • Tumia Camera ya Simu janja yako kama Mkalimani wako.

 

Teknolojia inabadilisha dunia kwa kasi bwana au sio ukiwa na App ya google Translate, ambayo inaweza kutafsiri lugha 29 utafanikisha hilo kuweka kamera mbele ya maandishi yaliyoandikwa na  hapo App itafanya zoezi zima la kutafsiri kwenda katika lugha unayoitaka.

  • Tumia kama camera ya ulinzi

 

Ulishawahi kuwa na hamu ya  kutumia kamera ya simu yako kama njia ya ulinzi? Labda una kamzigo kako pale na unataka ukachunge bwana usihofu mambo yanwezekana kua App maalum ambazo zinakuwezesha kufanya hayo yote.

App hizi hutumia kamera ya simu janja ili kugundua mwondoko wa iana yeyote(motion) na kisha kukutaarifu kupitia barua pepe yaani (email) yako.

Kwa android shusha App ya Silent  Eye shughuli imeisha hapo.

 

  • Shangaa anga

Hivi ushawahi kuapata kimehemuhe usiku ukawa unashangaa anga na ukaanza kujiuliza maswali kama baadhi ya vitu unavyoviona ni nyota au sayari zingine?

Nikufahamishe tu App ya Skyview kwa Android na iOs itakupa majibu yote.

kadhaa

 

App hii inatumia kamera ya simu yako katika kukuonyesha jinsi anaga ilivyo chakufanya sasa hakikisha unaelekeza kamera ya simu yako katika anga utaona mambo yanavyokwenda.

Ebwanaa hivi uliyajua matuzi haya ya camera kwenye simu janja yako? Au ndo ulikua unapambania kupiga picha tu hahhaha chukua na hayo sasa This is Smartphone bhanaaa!!!!!!!!!!!.

 
Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on Career and skills development every Monday and entertainment, every Friday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include SMARTPHONE and NIPE DILI.

Latest Post