Wole Soyinka amkingia kifua Davido

Wole Soyinka amkingia kifua Davido

Baada hivi karibuni mwanamiziki kutoka nchini Nigeria #Davido ku-post video ya wimbo wake mpya ukiwa una mahadhi ya dini ya kiislamu na kupelekea wafuasi wa dini hiyo wamjie juu kwa madai ya kuwa ameidhalilisha dini yao, huku wakimtaka afute video ya wimbo na kuwaomba msamaha hadharani.

Mtaalamu wa fasihi, prof. #WoleSoyinka amesema kuwa ‘staa’ huyo wa muziki hana kosa kwa waislamu mpaka wamtake aombe msamaha.

Katika utetezi huo Wole Soyinka alimshutumu gavana wa zamani wa jimbo la kaduna, Nasir El Rufai kwa kudai kuwa tukio kama hili liliwahi kufanyika siku za nyuma na gavana huyo kwa kuwadhalilisha wakristo lakini kamwe hakutakwa kuomba msamaha.

Mbali na hilo pia alikumbusha kuhusu tukio la wanafunzi wa kiislamu kumuua binti aitwaye Deborah Yakubu ambaye alikuwa akisoma kwenye chuo cha kikristo kwa madai ya kuwa amefanya kitendo cha kukufuru.

Hadi sasa msanii Davido amepoteza followers zaidi ya 30,000 katika ukurasa wake wa instagram, huku baadhi ya mabango yenye picha zake yakichomwa moto Nigeria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags