Mkali wa Afrobeat Wizkid ni miongoni mwa wasanii walioingai kwenye historia ya marehemu mwanamuziki wa reggae Bob Marley baada ya albam ya msanii huyo aliyefariki mwaka 1981 kuondoka na tuzo ya Grammy 2025.
Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Bob umechapishwa ujumbe wa kutoa shukrani kwa Wizkid, Bloody Civilian na wengine kwa mchango wao katika kufanikisha albamu iliyopewa jina la ‘Bob Marley One Love Music Inspired by Film’ kuondoka na tuzo hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Marley
“Bob Marley One Love Movie, Music Inspired By The Film’ ilishinda tuzo ya Albamu Bora ya Reggae katika Grammys. Hongera kwa wasanii wote wakubwa waliosaidia kutengeneza albamu hii, na heshima kubwa kwa wanachama wa @recordingacademy kwa kutambua kazi hii, “imeeleza taarifa hiyo.
Albamu hiyo ilitolewa kama sehemu ya kuadhimisha urithi wa Bob Marley ikiwa na filamu inayohusiana na maisha yake na muziki wake. iliunganisha wasanii mbalimbali ambao waliimba nyimbo za Bob kisasa zaidi huku ikiwa na mchanganyiko wa reggae, Afrobeats, na R&B.
Bob Marley alizaliwa Februari 6, 1945 na alifariki dunia 11 Mei 1981 akiwa na umri wa miaka 36, kwa ugonjwa wa saratani ya ngozi ambayo ilianzia kwenye kidole chake cha mguu na kusambaa mwili mzima.
Leave a Reply