Will Smith na Mkewe wanunua nyumba billion 26

Will Smith Na Mkewe Wanunua Nyumba Billion 26

Niaje wanaa leo kwenye gumzo mitandaoni bwana hatari na nusu, wewe ukisema huna hela l kaa ujifikirie mwenzangu na mie unakwama wapi, Mwigizaji na staa nchini Marekani, Willard Carrol maarufu kama Will Smith na mkewe Jada Pinkett maarufu kama Jadasmith wamenunua jumba la kifahari linalo gharimu $11.3M ni sawa na Billion 26 za kitanzania.

Wawili hao wanatajwa kuwa na mijengo zaidi ya nane nchini humo ukiachilia mbali nyumba walioinunua huko Hidden Hills Califonia, nyumba hiyo inatajwa kuwa na vyumba vya kulala 6, mabafu 6, swimming pool na sehemu 4 za kupark magari.

Smith anatarajia kuzindua kitabu chake  November 9 mwaka huu ambacho amekipa jina la “Will Smith an evening of stories with friend” alifunguka kupitia ukurasa wake na kueleza kuwa “I know it’s my birthday, but being able to see y’all in person again is the gift!! Philly, NYC, Chicago, LA and London… see you in November” alisema
Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on Career and skills development every Monday and entertainment, every Friday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include SMARTPHONE and NIPE DILI.

Latest Post