Will Smith ampiga kofi Chris Rock jukwaani

Will Smith ampiga kofi Chris Rock jukwaani

Usiku wa kuamkia leo nchini Marekani zilitolewa tuzo za filamu za Oscar na moja ya story ambayo imezua gumzo mitandaoni ya mwigizaji Will Smith baada ya kumpiga kofi mchekeshaji Chris Rock aliyefanya utani kwa kumcheka mkewe Jada Smith kuwa na kipara.

Unaambiwa kwamba Will Smith alikasirishwa na utani huo kwa sababu mkewe ana tatizo la kiafya ambalo limesababisha nywele zake kukatika.

Baada ya tukio hilo Will Smith alikuja kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mwigizaji bora na akatumia nafasi hiyo kuomba msamaha kwa kitendo alichokifanya.

Hata hivyo Chris Rock alimsamehe Will na utani baina yao ukaendelea wote wakifurahi.

Itakumbukwa kwamba Jada Smith alishawahi kuweka wazi kuwa anapambana na ugonjwa wa alopecia ambao husababisha nywele zake kukatika.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags