WFP kuchunguza uuzwaji wa chakula cha msaada

WFP kuchunguza uuzwaji wa chakula cha msaada

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), linachunguza wizi wa chakula cha msaada kupitia operesheni za kiutu nchini Ethiopia, hii ikiwa ni kulingana na barua ambayo shirika la habari la AP liliipata.

Barua hiyo iliyoandikwa na mkurugenzi wa WFP nchini humo Claude Jibidar na kutumwa kwa washirika wake kwenye taifa hilo, ambako watu milioni 20 wanategemea misaada kutokana na ukame mkali.

Aidha barua hiyo imeonya juu ya mauzo yanayotia wasiwasi ya chakula cha msaada na kutaka kuchukuliwa hatua ili kuzuia matumizi mabaya ya msaada nchini humo.

Jibidar amewatolea wito washirika wake kushirikishana taarifa zozote ama visa vya matumizi mabaya ya chakula hicho vinavyowasilishwa na wafanyakazi wao, watumiaji ama mamlaka ya maeneo husika, ingawa barua hiyo haikutaja kisa chochote.

Chanzo DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags