Wezi walioiba choo cha dhahabu kizimbani

Wezi walioiba choo cha dhahabu kizimbani

Wanaume wanne wameshtakiwa kwa wizi wa choo cha dhahabu chenye thamani ya £4.8 milioni katika jumba la #Blenheim, #Oxfordshire nchini #Uingereza.

Wizi huo ulifanyika Septemba mwaka 2019 ambapo wezi hao watafikishwa katika mahakama ya #Oxford Novemba 28, mwaka huu kwa ajili ya kusomewa hukumu yao.

Ambapo wawili kati yao wanakabiliwa na mashtaka ya wizi na wawili wengine wanatuhumiwa kula njama ya kuhamisha mali iliyoibiwa.

Choo hicho ambacho kilikuwa sehemu ya maonyesho ya msanii wa #Kiitaliano #MaurizioCattelan na kilikuwa kinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa hivyo kulikuwa na kikomo cha muda wa kutumia wa dakika tatu ili kuepusha foleni ambapo #choo hicho kilitumika siku mbili tuu kabla ya kuibiwa.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post