Wema: Whozu ukiniacha waje wanizike

Wema: Whozu ukiniacha waje wanizike

Alooooh! Mapenzi yametaradadi huku upande wa pili kwa madame mwenyewe, Wema Sepetu, basi bwana kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa mpenzi wake ambae ni msanii wa bongo fleva Whozu kuwa akimuacha wamzike tuu maana si kwa huba analopewa.

Ujumbe huo ukiwa umeambatanishwa na picha ya mwanamuziki huyo na kueleza kuwa, 'His lips, chibaba wangu mimi' na whozu alimjibu, 'my happiness, my soul, my chimama, nakupenda sana.'

Basi bwana mlimbwende huyo baada ya kuitwa majina mazuri hakukaa kimya aliamua kujibu komenti ya Whozu na kusema kuwa, “ukiniacha wanizike yaani waje wanizike tuu.”

Inaonesha hili ndio penzi lenye nguvu zaidi kwa Wema kiasi kwamba yuko tayari kufa akiachwa na mwanamuziki huyo. Je mwanangu sana wa Mwananchi Scoop uko tayari kufa kwa ajili ya chimama/ chibaba wako? Dondosha komenti yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags