Wema sepetu: Filamu za tanzania hazitakuwa kama zamani tena

Wema sepetu: Filamu za tanzania hazitakuwa kama zamani tena

Baada ya mwigizaji mkongwe na aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu kufika nchini Korea kwa ajili ya ziara ya mafunzo kuhusiana na mswala mazima ya tasnia ya uigizaji, mwigizaji huyo ameahidi kuwa filamu za Tanzania hazitakuwa kama zamani.

Wema ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram wakati alipokuwa kwenye studio za Sinema kwa kueleza kuwa amefurahishwa na amejifunza vingi katika studio hizo.

“Leo tukaenda huko Maajabu ya Cinema za Korea yanapofanyika, ni uzoefu wa Kipekee maishani mimi binafsi nilifurahia kila dakika, Filamu za Tanzania hazitakuwa kama zamani tena wallahi, Mama anatimiza Tunasogea” ameandika Wema

Utakumbuka kuwa Wema ameongozana na wasanii wenzie wa filamu Tanzania kwenda Korea kwenye ziara yao ya kujifunza mambo ya filamu.

Baadhi ya mastaa wa filamu ambao wapo kwenye ziara hiyo ni Irene Paul, Wema Sepetu, Idris Sultani, Dorah, Johari Chagula, Gabo Zigamba, Steve Nyerere, Eliud Samwel, Getrude Mwita na Godliver Gordian.

Wema Sepetu amewahi kuonekana katika filamu kama ‘Chungu cha Tatu’, ‘Madame’, ‘Shabiusi’, ‘Mapenzi Yamerogwa’ ‘More Than Woman’ na nyinginezo nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags