Wema Sepetu ataja kilichomuingiza mkenge hadi kufilisika

Wema Sepetu ataja kilichomuingiza mkenge hadi kufilisika

Duh! Embu tukae chini na tusikitike kidogo, nyie nyie kumbe watu wana stori nzito kama hizi ni vile tu hatujakaa nao vizuri. Basi bwana kama kawaida yetu kila siku tunakusogezea yale mastori makubwa, na leo tumeangukiwa kwa the Tanzanian sweatheart, Wema Sepetu.

Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na mijadala mingi kuhusiana na mwanadada huyo juu ya kufilisika kwake. Watu wakataka kujua ni nini kilimsibu, leo Mwananchi Scoop tunakushushia nondo hii kujua ni kitu gani kilimkumba mrembo huyo mpaka kufikia hivyo.

Kupitia mahojiano na tv ya mtandaoni inayoongozwa na msemaji wa zamani Yanga, Haji Manara, mwanadada huyo aliulizwa swali na kutajwa kuwa na pesa nyingi hapo awali lakini kushindwa kununua Range Rover, kuwa na mjengo mkubwa kama mastaa wengine na kueleza kuwa…

“Siwezi kusema kuwa matuminzi yangu mimi yamenifanya nisiweze kuwa na Range au nisiweze kuwa na jumba kubwa, huwa naishi maisha yangu halisi, pale ninapokuwa ninacho basi ninacho na nikiwa sina basi sina,” alieleza Mwanadada huyo ambaye amewahi kuwa kimwana wa Diamond Platnumz.

Aliendelea kwa kusema kuwa “Wakati watu waliniona nashika sana pesa, na kweli nilikuwa na pesa lakini niliingia mkenge nikaingia katika masuala ya kugombea ubunge, ilinirudisha sana nyuma na matumizi yangu hayajanirudisha nyuma ila kule nilipo kwenda kugombea niliwekeza zaidi ya milioni 320,” amesema Wema Sepetu

Haya wale wadau mliokuwa mnajiuliza mwanadada huyu ni kipi kimemfanya mpaka afirisike arudi tena chini ni kuhusiana na mauala ya kuingizwa chaka katika kugombea, alimalizia kwa kueleza kuwa…

“ Kutokana na jambo hilo nikajikuta nimerudi nyuma kabisa kwasababu ile ilikuwa ni kama bahati nasibu nilizani nitapata lakini sikupata, lakini sikuichukulia kama ni kitu kikubwa kwasababu kila kitu kinatokea kwa sababu,” amesema Wema.

Funzo, katika story hii ya leo watu mjifunze kupitia mrembo huyu najua wengi sana wamepitia hii changamoto kutokana na mkenge wanaoingizwa, haya uchaguzi unakaribia so akili kichwani kwako utachagua kunyoa ama kusuka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post