Waziri mkuu amuachisha kazi mwanae

Waziri mkuu amuachisha kazi mwanae

Waziri Mkuu kutoka nchini Japani, Fumio Kishida amechukua uamuzi wa kumuondoa mtoto wake katika cheo chake cha katibu mkuu kutokana na kuonesha tabia isiyofaa katika jamii.

Hatua hiyo ameichukua baada ya kuvuja kwa picha ambazo zilikuwa hazina maadili zikimuonesha kijana huyo akisherekea sherehe za mwisho wa mwaka pamoja na ndugu zake katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu.

Kishida alisema amechukua uamuzi huo ili kuonesha uwajibikaji kwa kijana wake na watu wengine wakifanya vitendo vilivyotafsiriwa kuwa utovu wa nidhamu.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post