Wazee watishiwa kifo kwasababu ya urithi

Wazee watishiwa kifo kwasababu ya urithi

Kufuatiwa na wimbi kubwa la malalamiko ya vikongwe kuhusu kulazimishwa kutoa urithi kwa watoto wao huko mkoani Shinyanga baadhi ya wazee wanadai kuwa wamekuwa wakitishiwa na wakiuwawa, kwa kukataa kutekeleza matakwa ya watoto wao ya kutaka urithi na kuwatengenezea vifo vya imani ya kishirikina.

Katibu wa baraza la wazee la Halmashauri hiyo, Laurent Nkwambi anasema,

“Manispaa hii ina jumla ya wazee 6,692 huku 50% wakiishi maeneo ya pembezoni ambako ndipo kunafanyika vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na mauaji, yote yanasababishwa na watoto kutaka mgawo wa mali yakiwemo Mashamba” alisema Katibu huyo.

Mbali na tukio hilo kumekuwa na matukio mbalimbali ya udhalilishaji mkoani humo ikiwemo unyanyasaji wa kingono kwa wanawake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags