Wazazi wa Diaz wadaiwa kutekwa

Wazazi wa Diaz wadaiwa kutekwa

Wazazi wa mchezaji nyota wa ‘klabu’ ya #Liverpool, #LuisDiaz wanadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wakati wakiwa kwenye gari kuelekea nyumbani kwao Mjini Barrancas, nchini Colombia.

Inaelezwa kuwa watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki waliivamia familia hiyo na kuwachukua kwenye gari lao na kuwapeleka kusikojulikana.

Hata hivyo, Rais wa Colombia, Gustavo Petro amethibitisha kwamba mama wa mwanasoka huyo wa Colombia, Cilenis Marulanda ameokolewa huku maofisa wakiendelea na msako kumtafuta baba yake ambaye bado hajapatikana mpaka sasa.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyejiunga na Liverpool Januari 2022 akitokea FC Porto ya Ureno bado hajazungumzia tukio hilo lakini Shirikisho la ‘Soka’ nchini Colombia katika taarifa yake limesikitishwa utekaji nyara huo na kuzitaka mamlaka husika kumuokoa baba wa mshambuliaji huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags