Wawili wafariki wakati wakidaka kumbikumbi, Kigoma

Wawili wafariki wakati wakidaka kumbikumbi, Kigoma

Watu wawili wenye umri kati ya miaka 18 na 20 wamefariki dunia baada ya kugongwa na Bodaboda wakati wakikamata Kumbikumbi katika kichuguu pembezoni mwa barabara katika Kijiji cha Mahembe Mkoani Kigoma.

Waliofariki ni Siya Ramadhani na Neema Moshi ambapo walikuwa na wenzao kabla ya mwendesha Bodaboda huyo kuacha njia na kuwagonga na kusabisha majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na kupelekea kifo.

Polisi Mkoani Kigoma  wanamshikilia Dereva aliyewagonga Yeovan Kagizo( 28 ) ambaye anatuhumiwa kusabanisha vifo vya Wasichana hao kutokana na mwendokasi.

Kumbikumbi hao hutumiwa kama mboga kwenye chakula katika maeneo hayo kama ilivyo katika maeneo mengine na hupatikana maara baada ya mvua kunyesha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags