Waumini wanne wafariki  wakiwa wamefunga

Waumini wanne wafariki wakiwa wamefunga

Watu wanne ambao ni waumini wa Kanisa la Good News International Church   walipatikana Alhamisi wakiwa wamefariki na wengine zaidi ya kumi wamelazwa hospitalini katika kaunti ya pwani ya Kilifi nchini Kenya, baada ya kuokolewa wakisubiri mwisho wa dunia unaokaribi.

Polisi walisema kundi hilo lilipatikana katika msitu walimokuwa wakiishi kwa siku kadhaa baada ya kuambiwa na mhubiri wa eneo hilo kufunga huku wakingoja kukutana na yesu.

Polisi nchini humo walisema wataanza tena msako wa kuwatafuta wanachama zaidi wa kundi hilo leo ijumaa asubuhi kufuatia ripoti kwamba wengine walikuwa bado msituni. Huku kukiripotiwa kupata kaburi msituni.

Kanisa hilo linaloongozwa na mchungaji wa eneo hilo ambaye amekuwa chini ya polisi kwa madai ya kuwataka waumini wake kufa njaa ili kufika mbinguni kwa kasi.

Aidha kwa sasa mhubiri huyo yuko huru baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya polisi baada ya kushtakiwa mwezi uliopita kuhusu kifo cha watoto wawili ambao wazazi wao ni miongoni mwa wafuasi wake.

Chanzo BBC

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags