Wauguzi wagoma nchini Uingereza

Wauguzi wagoma nchini Uingereza

Maelfu ya wauguzi kwenye hospitali za nchini Uingereza wameanza mgomo mkubwa kudai nyongeza za mishahara.

Manesi wanashiriki kwenye mgomo huo katika maeneo yote ya England, Wales na Ireland Kaskazini. Mgomo huo ni wa kwanza kufanyika katika historia ya miaka 106 ya Jumuiya kuu ya Umoja wa Manesi nchini Uingereza.

 Wauguzi hao wanadai nyongeza ya mishahara ya asilimia 20. Hata hivyo serikali ya Uingereza imesema haina uwezo wa kutoa nyongeza ya kiwango hicho.

Jumuiya hiyo inataka nyongeza itakayovuka kiwango cha mfumuko wa bei kilichofikia asilimia 11 mwezi uliopita nchini Uingereza. Kwa mujibu wa takwimu mishahara ya wahudumu hao imeanguka kwa asilimia 20 tangu mwaka 2010 kutokana na kumezwa na mfumuko wa bei.

Katibu mkuu wa jumuiya ya manesi ameitaka serikali ichukue hatua zaidi ili kuwazuia manesi kuacha kazi ya uuguzi na kwenda kwingineko. Kwa sasa pana uhaba wa manesi 50,000 nchini Uingereza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags