Wauguzi wafutiwa leseni kwa kusababisha kifo cha Mjamzito

Wauguzi wafutiwa leseni kwa kusababisha kifo cha Mjamzito

Taarifa hii imetokea huko mkoani Mtwara ambapo Baraza la Wauguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limefanya uwamuzi huo kwa wauguzi wasaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkomaindo, Masasi ambao ni (Elizabeth Njenga na Pascal Mnyalu) kutokana na uzembe uliosababisha kifo cha Mjamzito na Mtoto wake.

Aidha Wauguzi wengine Joyce Nkane na Tumaini Milanzi wamepewa onyo kali huku Lucia Liababa akifutiwa shtaka baada ya kuonekana kutohusika moja kwa moja

Hata hivyo Madaktari wawili, Amina Mushi na Hashimu Chiwaya ambao nao walishtakiwa, taarifa zao zitapelekwa kwenye Baraza la Madaktari ili hatua stahiki zichukuliwe.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags