Watu 28 wafariki katika kimbunga, Bangladesh

Watu 28 wafariki katika kimbunga, Bangladesh

Idadi ya watu waliokufa kutokana na Kimbunga Sitrang nchini Bangladesh imefikia 28 huku mamilioni ya wengine wakisalia bila umeme.

Idadi hii imeongezeka baada wafanyakazi wa uokoaji wa Bangladesh kuipata miili ya wafanyakazi wanne waliotoweka kwa boti. Kimbunga Sitrang kilipiga kusini mwa Bangladesh siku ya Jumatatu huku serikali ikisema karibu nyumba 10,000 na mazao katika maeneo makubwa ya mashamba yakiharibiwa wakati ambapo nchi hiyo ikikumbwa na mfumuko wa bei ya vyakula.

Vimbunga ni tishio la mara kwa mara katika eneo hilo lakini wanasayansi wanasema huenda mabadiliko ya hali ya tabia nchi ikawa sababu ya kutokea mara kwa mara kwa dhoruba hizo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags