Watu 109 wamefariki kutokana na maporomoko Rwanda

Watu 109 wamefariki kutokana na maporomoko Rwanda

Shirika la habari la serikali nchini Rwanda limeripoti kwamba watu 109 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi huko Mahgaribi na Kaskazini mwa Rwanda.

Maporomoko hayo ni kutoka milimani na kufunga barabara pamoja na kuharibu makao ya watu hali hiyo ili tokana mvua kubwa zilizoanza kunyesha siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni.

Gavana wa mkoa wa Magharibi Francois Habitegeko amesema kwamba maafisa wanafanya kila juhudi kufikia kila nyumba iliyoharibiwa na kuhakikisha kwamba hakuna mtu aliyekwama kwenye nyumba hizo.

Aidha baadhi ya watu wameokolewa na kupelekwa hospitalini mpka sasa maafisa wajasema idadi ya watu waliolazwa hospital. Watabiri wa hali ya hewa wametabiri kwamba mvua kubwa itaendelea kunyesha mwezi huu wa mei, katika nchi za Afrika mashariki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags