WaterAid yakabidhi vituo 12 vya kunawia mikono vyenye thamani ya Sh 144 Milioni

WaterAid yakabidhi vituo 12 vya kunawia mikono vyenye thamani ya Sh 144 Milioni

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Rashid Mfaume amesema kuwa unawaji sahihi wa mikono unasaidia kuepusha vifo vitokanavyo na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na kuhara kwa asilimia 35.

Aisha amesema unawaji huo pia usaidia kupunguza vifo vitokanavyo na maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa hewa ikiwemo Uviko 19 kwa asilimia 322.

Dk. Mfaume amebainisha hyao jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa vituo 12 vya kunawia mikono vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la WaterAid kwa kushirikiana na The Foreign, Commonwealth & Development Office (FCDO) na Unileve kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya kunawa mikono.

Rashid Mfaume amesema Serikali itaendelea kuwekeza nguvu katika unawaji sahihi wa mikono na hiyo itasaidia kuepuka vifo vya magonjwa hayo kwa zaidi ya asilimia 67 hivyo ameitaka jamii kuendelea na utaratibu huo kwa lengo la kujikinga na maradhi hayo.

Amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana bado eneo hilo la unawaji wa mikono linapewa nafasi ndogo katika baadhi ya maeneo hivyo amehimiza jamii kuendelea kunawa ili kujikinga na magonjwa yanayoambukiza.

Naye Mkurugenzi Mkaazi wa WaterAid, Anna Mzinga amesema katika jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia watanzania kunawa mikono ili kupambana na maambukizi ya Uviko 19, wametoa vituo hivyo 12 vilivyojengwa maeneo mbalimbali ya mkoani Dar es Salaam na vimegharimu jumla ya Sh.144 Milioni.

Amesema maeneo yaliyonufaika na vituo hivyo ni Hospitali ya Mwananyamala, Mnazi Mmoja, Temeke, Kituo cha Magufuli,  Shule ya Msingi Malamba Mawili na Msasani, Stendi ya mabasi mawasiliano na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Amesema msaada huo umetolewa na shirika lao kwa kushirikiana na Shirika la The Foreign, Commonwealth and Development Office (FCDO) na Unilever ambapo wametoa msaada huo kwa lengo la kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano ya Uviko 19.

"Tunatambua kuwa pasipo huduma sahihi ya maji, usafi wa mazingira na vifaa vya kunawia mikono kwenye makazi yetu, shuleni, vituo vya kutolea huduma za afya na taasis nyingine basi mazingira yetu yatakuwa ni vyanzo vya magonjwa na kuacha jamii ikiwa katika hatari ya kupata milipuko ya magonjwa ya kuambukiza na kuingia kwenye gharama kubwa za matibabu, " amesema

Hata hivyo amesema akiondoa afua nyingine, watu wengi ni mashahidi namna unawaji wa mikono ulivyoongezeka nchini  hali iliyosaidia katika mapambano dhidi ya Uviko 19.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags