Kufatiwa na mapigano huko nchini Sudani wanafunzi 150, watumishi wa ubalozi 28 na diaspora 22 wa Kitanzania wanatarajiwa kuwasili leo Aprili 27 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Baada ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Dkt. Stergomena Lawrence Tax kupokea taarifa katika serikali ya Sudani kuwa raia wakigeni waliopo nchini humo kurudi katika nchi zao kwa kindi hiki cha mapigano kwaajili ya usalama.
Hatua ya kuwatoa Sudan ni kutokana na mapigano ya kuwania madaraka yanayoendelea baina ya Jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha Msaada wa Haraka RSF.
Aidha, raia wa nchi nyingine waliosafirishwa kwa mabasi kwa siku mbili kutoka Khartoum, AlQadarif, Metema hadi Gondar watakabidhiwa kwa Balozi zao huko Addis Ababa ili warudi kwao kwanza.
Leave a Reply