Watano wanyongwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya

Watano wanyongwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya

Serekali nchini Iran imetoa hukumu ya kunyongwa kwa watu watano siku ya jana jumatatu kwa kufanya ulanguzi wa  dawa za kulevya kwa kutumia silaha kusini mwa nchi hiyo.

Washukiwa hao wote ambao wametajwa kama wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya wenye silaha walikuwa wamehukumiwa kifo kwa kunyongwa.

Katika hukumu iliyoidhinishwa na mahakama ya juu ya Iran, tovuti ya mahakama ya Mizan Online ilimnukuu Mojtaba Ghahramani, Jaji Mkuu wa jimbo la kusini la Hormozgan.

Lakini Mojtba aliongeza kusema kwamba hukumu za watu waliotajwa zilitekelezwa asubuhi ya Jumatatu katika magereza ya Bandar Abbas na Minab ya Hormozgan.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags