Watumishi watatu wa Hospitali binafsi ya Sakamu iliyopo mkoani Geita wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi kufuatia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha watumishi wawili wakimpongeza mwenzao kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutumia majitiba maarufu ‘dripu’.
Akizungumza na Mwananchi Digital, Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk Salvatory Msimu amesema tukio hilo limetokea kwenye hospitali yake na sio kwenye kituo cha afya Nyankumbu kama ilivyosemekana awali.
“Ni kweli tumefuatilia tumeona ni watumsihi wetu na ninaandaa taarifa kwa umma kuwajulisha kuwa sio Nyankumbu kama ilivyosemakana lakini ni kwetu na hatua zetu kama taasisi tulizochukua ni kuwaandikia barua ya kuwasimamisha wakati ambao uchunguzi unaendelea.
Kuhusu siku ya tukio, Dk Msimu amesema mpaka sasa hawajajua lilitokea lini lakini timu iliyoundwa itatoa majibu wakati watakapokamilisha uchunguzi.
Cc: Mwananchi
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply