Wasanii wa filamu Bongo watua Korea

Wasanii wa filamu Bongo watua Korea

Wasanii wa filamu Tanzania wamewasili Korea kwenye ziara yao ya kujifunza mambo ya filamu.

Baadhi ya mastaa wa filamu ambao wapo kwenye ziara hiyo ni Irene Paul, Wema Sepetu, Idris Sultani, Dorah, Johari Chagula, Gabo Zigamba, Steve Nyerere, Eliud Samwel na Godliver Gordian.

Wasanii hao wametoa shukrani kufika Korea na kutembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea ambapo wameweza kukutana na balozi wa Tanzania nchini Korea, Togolani Mvura.

“Mapema leo na muheshimiwa mwenye dhamana ya ubarozi nchini Korea na watu wake wenye moyo wa shukrani katika ziara chanya, tumepata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea tukiwa kwenye ziara yetu, we are very humbled,” wameeleza

Ikumbukwe kuwa dirisha hilo la wasanii kufika Korea lilifunguliwa na Rais Samia Juni 1, 2024 baada ya kuwakutanisha Watayarishaji wa Filamu wa Korea, Waandaaji na Waigizaji wa Filamu wa Tanzania Jijini Seoul, kujadli mambo mbalimbali yanayohusu Tasnia ya sanaa na kubadilishana ujuzi kwa lengo la kujifunza.

Hayo yalijiri katika ziara rasmi ya kikazi aliyoenda Rais Samia Suluhu Hassan Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea, mwezi Mei mwaka huu, akiwa ameongozana na wasanii wa Tanzania akiwemo waigizaji Elizabeth Michael (Lulu) na Vyone Cherrie (Monalissa) huku kwa upande wa waandaji wa filamu akiwemo Leah Mwendamseke (Lamatha).
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post