Wasanii na mavazi ya ajabu

Wasanii na mavazi ya ajabu

Kawaida maisha ya baadhi ya wasanii ambayo wanayaonesha kwenye mitandao ya kijamii huwa ya kustaajabisha, kumekuwa na ubunifu wa vitu mbalimbali ambavyo wanavifanya kwenye upande wa mavazi na kupelekea wengi kushangaa uvaaji wao.

Leo tuangalie mavazi ya ajabu ambayo wasanii na watu maarufu duniani wamewahi kuyavaa,

Kwa upande wa #Bongo matukio hayo yamekuwa hayajitokezi sana lakini tukumbuke vazi alilowahi kuvaa nyota wa muziki nchini Diamondplatnumz ambalo lilikuwa limetengenezwa kwa kutumia mifuko  ambayo inafahamika kwa jina maarufu kama “Shangazi Kaja.”

 Nchini Kenya kutana na mchekeshaji Erick Omondi ambaye mara nyingi amekuwa akionekana katika mavazi ya kushangaza, nikukumbushe aliwahi kutinga Tanzania na vazi la ajabu na viatu vikubwa  miguuni, lakini pia amewahi kwenda nchini Uganda na vazi la mifuko huku akitumia usafiri wa gari dogo lenye muundo wa kiatu, kuvaa majani na nywele.

Jambo hilo halijaishia tu East Africa siku sio nyingi ameonekana msanii kutoka Nigeria Burna Boy akiwa ndani ya vazi ambalo wengi walishindwa kuelewa kama vazi lile ni sketi, gauni au suruali.

 Kwa upande wa Marekani tumtazame mwanamuziki Kanye West ambaye mara nyingi amekuwa akionekana ndani ya mavazi yenye kushangaza, na hivi juzi kati ameanza utaratibu mpya wa kutembea bila viatu miguuni.

Kwa upande wako na wewe tuambie vazi gani la ajabu kutoka kwa msanii lilikushangaza ?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags