Wapendanao mwenye tattoo mwili mzima wafunguka

Wapendanao mwenye tattoo mwili mzima wafunguka

Kuna msemo unasema utampata mweza wa kufanana naye, hivi ndivyo ilivyo kwa wapendanao Nes na Joel ambao walipendana kutokana na wote kupenda kuchora tattoo.

Ikiwa jana ni siku ya Valentine wawili hao walifunguka katika #InkedMagazine, njinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza na changamoto walizo pitia kila mmoja ambapo walieleza kuwa haikuwa rahisi kuwa pamoja.

Nes aliweka wazi kuwa alitokea katika familia ya kijeshi na aliwahi kutumikia jeshi la Marekani kwa muda lakini alishindwa kuendelea kutokana kuingia katika uchoraji wa tattoo ambapo ilisababisha iwe ngumu kupokelewa katika familia yake tena.

Huku kwa upande wa mwanammme wake Joel alieleza kuwa kwake maisha hayakuwa magumu kama ya mpenzi wake kwani toka alivyokuwa mdogo alipendelea kuchora hivyo akaona aanze kazi ya kuwa mchoraji wa tattoo.

Wawili hao ambao hawakuweka wazi mwaka waliyo anzisha mahusiano yao walieleza kuwa urembo wa tattoo umeshika sehemu kubwa ya maisha yao ndiyo maana kila baada ya muda fulani huchora tattoo mpya.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags