Wanyama wenye vichwa viwili

Wanyama wenye vichwa viwili

Ni ajabu na nadra sana kuona viumbe wenye vichwa viwili, kwa haraka unaweza dhani upo ndotoni, lakini ukweli ni kwamba viumbe wa aina hiyo wapo na wanaishi kama waishivyo wengine, leo hii wafahamu viumbe hao wenye vichwa viwili.

Lakini kabla sijakujuza juu ya viumbe hao jiulize ni mara ngapi umewahi kuona viumbe wa aina hiyo? kama ulikua huamini kuhusu hilo basi amini kwamba viumbe hao wapo na wanaishi, kwa leo tuanze na hawa.

Nyoka mwenye vichwa viwili, wapo nyoka wa aina hii ambao hujulikana kwa jina la Double Dave, nyoka wa aina hii kwa mara ya kwanza walionekana nchini Marekani, na inaelezwa kuwa nyoka hawa huwa na sumu kali , vichwa viwili macho manne na ndimi mbili ambazo hufanya kazi tofauti.


Kobe wenye vichwa viwili, aina hiyo ya #Kobe huitwa tortoise Janus, kwa mara ya kwanza Kobe wa aina hii kuonekana alichukuliwa na kutunzwa kwenye jumba la makumbusho ya kihistoria litwalo, Geneva Museum of Natural History’s.



Papa mwenye vichwa viwili, kwa mara ya kwanza alipatikana mwaka 2013 Ghuba ya Mexico wataalam wanaeleza kuwa Papa wa aina hii huanza kuungana kwanzia akiwa yai ambavyo muunganiko huo husababishwa na kiwango cha joto kuwa juu.


Lakini sio hao tu bali kuna Paka mwenye vichwa viwili, japo kwa upande wake kuna utofauti kidogo kwani huwa na sura mbili na sio vichwa viwili kama ilivyo kwa viumbe vingine, midomo miwili, pua mbili, na macho matatu, Paka wa kwanza kuonekana kuwa na muonekano huo alifanikiwa kushika rekodi ya Dunia ya Guinness kama #Paka wa aina hiyo aliyeishi muda mrefu zaidi kwa sasa hayupo tena kwani alikufa mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 15






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags