Wanayokutana nayo wapangaji kwenye nyumba za kupanga

Wanayokutana nayo wapangaji kwenye nyumba za kupanga

Asilimia kubwa ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wanaishi kwenye nyumba za kupanga, lakini baadhi yao wamekuwa wakikutana na vioja mbalimbali kwenye nyumba hizo au kwa wenyenyumba wenyewe.

Utafiti uliofanywa na Mwananchi Scoop, kwa wapangaji katika maeneo mbalimbali umebaini kuwepo na kero nyingi wanazokabiliana nazo wapangaji, zikiwemo mashariti makali na mikataba bubu au isiyo rasmi kwa wapangaji.

Pia kumekuwa na tabia ya wenyenyumba ambao wanapangisha bila kuwaweka wazi wapangaji matatizo ya nyumba zao mpaka pale mpangaji anapolipia pesa au kuhamia kabisa, hivyo hupelekea wapangaji kupata shida na kushindwa kufanya maamuzi ya kuhama haraka kutokana na ugumu wa maisha.

Miongoni mwa kero wanazokutana nazo wapangaji kufukuzwa katika nyumba kabla ya mkataba kuisha, masharti makali katika nyumba kama vile kukataa wapangaji wenye watoto, kupika aina fulani ya vyakula na wapangaji wengine kubaguliwa kutokana na dini zao, miundombinu ya huduma za kijamii kuwa mibovu kama vile maji, choo, mpangaji kulipa zaidi pesa ya kodi kwa mmiliki kama kilinda usalama wa nyumba.

Na mara nyingi wenye nyumba huwa hawana habari ya kufanya marekebisho ya nyumba zao licha ya kuwa tayari wamepokea kodi, katika maeneo ya Mbagala ambapo ndiyo imekuwa sehemu yenye mkusanyiko wa watu wengi imebainika kuwa wenyenyumba ni wepesi kuwageuka wapangaji hatakama waliandikishiana kwenye mkataba.

“Unaweza ukakubaliana na mwenyenyumba ukaingia naye mkataba vizuri lakini baada ya siku chache anakwambia uondoke wakati ulishampa kodi ya miezi sita, yaani anaweza kukutafutia sababu yoyote tu” alisema Tabasamu Amuri mkazi wa mbagala.

Mpangaji mwingine aliyepanga maeneo ya Mbagala Chamanzi, Rehema Mohamed amesema kuwa, “kama mimi nilihamia nyumba ambayo ilikuwa inagombaniwa urithi na wamiliki basi hawakuwahi kutuambia mpaka pale tulipofikisha mwezi mmoja walituambia tuhame kinguvu ikiwa tumelipia kodi ya miezi sita, tukaanza kutishiwa kwa mauzauza ikabidi tuhame”

Rehema akamalizia kwa kusema imekuwa ikiwapa wakati mgumu na hasara za kifedha kama kuhamisha vyombo kila wakati husababisha vyombo kuharibika.

Funguka umewahi kukutana tukio gani kwenye nyumba za kupanga?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post