Wanawake wanaokula nauli kushtakiwa

Wanawake Wanaokula Nauli Kushtakiwa

Unamuomba mwanamke kuonana nae na unamtumia hela, halafu anakujibu "Utume na yakutolea," hayo ndio maisha ya wengi wetu, hasa wale tulio katika mahusiano?

Je hali inakuwaje pale ambapo ulimtumia na yakutolea akala nauli na asije? Vipi akikublock kabisa? Hapa ndipo ambapo wengine wanasema watakufanya kitu kibaya ama watakushtaki. Je hilo linawezekana?
 
Huko Jijini Nairobi nchini Kenya, Jaji wa Mahakama ameamuru mwanamke mmoja alipe fidia baada ya kula nauli ya mwanaume wake Ksh 3000 sawa Tsh 58,000 aliyomtumia kwa lengo la kukutana ambapo kutokufika kwake kulipelekea mwanaume huyo aende kumshitaki. Ametakiwa arudishe pesa hiyo Tsh 58,000 na nyongeza ya Ksh 20,000 sawa na Tsh 392,000 hivyo jumla atatakiwa kumlipa 450,000 kama fidia ya kumtesa kihisia mwanaume huyo.

Kwa nchi yetu ya Tanzania hali ni tofauti kidogo. Mwanasheria kuroka Avis Legal, Henry Mwinuka alisema kupitia mahojiano na runinga moja nchini kuwa, "Hapa Tanzania hakuna sheria ya kumuhukumu mwanamke baada ya kula nauli ya mwanaume baada ya kukubaliana kukutana na mwanamke hakutumiza ahadi, lakini sheria ya kanuni ya adhabu Sura ya 16 kuna kifungu kinazungumzia ni kosa la jinai Kwa mtu kufanya wizi wa kuaminika au wa kuaminiwa." 

Je kifungo hiko kinatosha kumuweka mwenzako ndani? Tupia comment yako!


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post