Wanaume wengi nchini Kenya wameanza kuvutiwa na upasuaji wa kufunga mirija ya mbengu za uzazi,Vasektomi. Haya ni kwa mujibu wa Marie Stopes nchini Kenya.
“Tumepokea maombi mengi kutoka kwa wanaume. Walakini, hatuwezi kufichua nambari hiyo kwa sababu ya usiri wa mteja.
Shirika hilo la kutoa huduma za Uzazi wa Mpango na Afya ya Uzazi wa Jinsia (SRH) linasema kuongezeka kwa hamu ya kutaka maelezo kunatokana na uelewa zaidi ambao umesababisha upatikanaji na matumizi ya huduma hizi.
"Kwa ujumla, Wakenya wamefahamu kuhusu majukumu sawa ya kijinsia na haja ya kuwa na mawasiliano zaidi kati ya wanandoa, tunazidi kuona wanaume wakichukua huduma za SRH” Mkurugenzi Marie Stopes Kenya Inviolata Wanyama alisema.
Chanzo BBC
Leave a Reply