Wanaochanganya shisha na dawa za kulevya kukiona

Wanaochanganya shisha na dawa za kulevya kukiona

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), imetangaza kuanza operesheni maalumu katika kumbi za starehe na ma-hoteli zenye Shisha ili kubaini wanaochanganya kiburudisho hicho na dawa za kulevya.

Taarifa ya operesheni hiyo imetolewa leo, Alhamisi Januari 25, 2024 na Kamishna Mkuu wa DCEA, Aretas Lyimo alipozungumza na waandishi wa habari.

Amesema watatembelea katika kumbi hizo na kupima mitungi kubaini kama kuna mchanganyiko na dawa za kulevya.

“Tutatembelea kumbi hizo tutapima mitungi ya shisha ili kubaini kama kuna uchanganyaji na dawa za kulevya na tukigundua tunawakamata wahusika,” amesema.

Amesema operesheni hiyo itahusisha ufuatiliaji wa matumizi na uzalishaji wa dawa za kulevya nchi kavu na majini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post