Wanafunzi wajiandae na maisha halisi baada ya kutoka vyuoni

Wanafunzi wajiandae na maisha halisi baada ya kutoka vyuoni

Na Michael Onesha

Aloooh! niaje niaje, wanafunzi wenzangu, ni ndugu yenu tena nimerudi na kitu new, kama tunavyojua wiki hizi ni wiki ambayo wapo baadhi ya wanafunzi wamemaliza mitihani yao na kumaliza chuo mazima, ambapo wanasubiri majibu na graduation ili kuhitimu mazima.
Basi ni time yao ya kurudi mtaani na kujua maana ya maisha magumu mtaani kutokana na yale wanayokuja kukumbana nayo, na siyo kama tunayakuza lakini hiyo ndiyo hali halisi. Haya ndiyo yatakusaidia wewe mwanachuo unayekaribia kuhitimu na kukufanya uone maisha mepesi kitaani.

•Hakikisha unatuma email kipofu.
Email kipofu ni zile email unazotuma kwa yeyote hujawahi kukutana nae. Unamjua waziri January Makamba lakini hujawahi kukutana nae, unamjua Zitto, unamjua Philip Mpango, kwenye mitandao haswa ya kijamii kuna emails zao hakikisha umetuma. Tuma kwa yeyote ambaye labda unamuheshimu, unamkubali, ni role model, unadhani utapata ushauri kutoka kwake, mtu ambaye unataka kusikia historia ya mafanikio aliyonayo.

Nijitolee mfano, wakati niko mwaka wa tatu, nilimtumia email Mchumi Mkuu wa IMF Gita Gopinath. Hi jina langu ni Kitumba mwanafunzi kutoka chuo kikuu Ardhi Dar es salaam Tanzania, nikamwambia kiukweli sijui naenda kufanya nini baada ya kumaliza masomo yangu lakini ningependa kuanzisha taasisi ya kufanya research yenye ukubwa kimataifa kama IMF nikamuomba anipe basics za kiutendaji.
Ingawa ilimchukua mwaka mzima kujibu, lakini email yake inanipa muongozo na confidence kiasi mpaka leo.
•Kuwa na marafiki 5 wazuri.
Angalia marafiki ambao mtasaidiana, kushirikiana na kupeana michongo pale itakapotokea, achana na marafiki ambao mkishamaliza chuo basi kila mtu anaenda kupambana na familia yake, marafiki wa kuambatana nao unawaona tuu ukiwa chuoni kutokana na matendo yao.



•Chukua kozi ya ujuzi wa vitendo.
Unaweza kuwa unasomea course yeyote ambayo binafsi umeichagua/ unaifurahia hiyo itakufanya ufaulu vizuri na ku-injoy muda wote utakaotumia chuoni lakini hakikisha unachukua kozi yeyote inayokupa ujuzi wa moja kwa moja mfano Computer science, mziki, uandishi, design, software, Lugha. Itakuongezea sifa za pekee huko mbeleni.

•Anzisha chochote.
Unaweza anzisha Club, NGO, Biashara hakikisha umeanzisha chochote ukiwa chuoni kwa sababu kubwa tatu. Mosi , Utaishi kiuhalisia zaidi. Vipi ukiwa unasoma halafu unayatenda hapo hapo yale unayoyasoma?. unajijengea mifano mingi ya moja kwa moja. Pili, ujasili na uzoefu. Utajua ni ugumu upi katika kuanzisha project na kuiongoza.

Binafsi niliwahi kuanzisha biashara ya sabuni wakati niko chuo. Niligundua kumbe kipawa changu cha kutunza fedha ni kidogo mno nilikua nauza kwa mkopo huku nikilipwa kidogo kidogo, wengine mpaka boom litoke sasa kwenye kuutunza mtaji najikuta nautumia tu.
Tatu, utaujua ukweli ya kwamba maisha baada ya shule siyo rahisi kihivyo kwenye chochote.

•Kuwa na ‘ze profesa’.
Ni wazi wanachuo mna tarajia kufika mahali fulani. Ze profesa ni rafiki yako aliye kwenye nyadhifa ya juu unayoitarajia kufika. Kama ni koneksheni au refarii ndiyo muda wako kumuandaa.

Kuna lecture ambaye ndiyo mkuu kwenye department ya kozi unayoichukua, ingawa ni mnoko fulani lakini msumbue. Hakikisha unamsumbua karibu kila siku ukimuulizia mambo kadha wa kadha atakuambia mengi, mfanye awe rafiki, utayajua mengi ambayo yanaweza kukusaidia katika maisha yako.

• Jitahidi usipitwe na mialiko yoyote
Mfano mzuri kwenye class tour, event za vijana, out na marafiki zitakusaidia sana kukutana na watu tofauti tofauti na kujifunza zaidi jinsi ya kuishi na watu.


•Omba kujitolea katika sehemu ya kazi yoyote.
Inauma kweli unamaliza chuo baada ya kuingia kazini unaingia kwenye internship huku ukilipwa nauli tu eti unatafuta uzoefu. Usiridhike na semister field kamwe, unachotakiwa kufanya baada ya kumaliza field ni kuendelea kukifanyia kazi kitu ulichosomea ili pindi itakapopatikana kazi unakuwa wa kwanza kuchaguliwa kutokana na uzoefu ulionao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post